Duration 41:27

Salama Na Baba Levo Ep 26 | ALL IN ALL Part 1

451 789 watched
0
4.6 K
Published 26 Jul 2020

#YAHStoneTown #SalamaNa #PodCast SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm� �� ‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru� �� GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack ‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa Kusema ukweli kabisa mimi na mgeni wetu wa wiki hii hatuna urafiki wala mazoea kabisa, ila tunafamiana kwa mbali na pengine (naamini) kila mmoja anamheshimu mwenzake kutokana na kazi ambazo kila mmoja wetu ameshafanya, na hiyo ndo ambayo imeleta heshima kati yetu. Pia tukumbuke heshima hainunuliwi wala haihongwi, huja yenyewe na kutuwama pale inapoona inafaa. Kwa kipaji na jina lake kuwa kule na huku nami ndo nilimfahamu Baba Levo. Utani wake kwa wasanii wengine (hasa siku za hivi karibuni) watanzania wamekua wakiuona sana. Ila kwa mujibu wa historia chache juu yake ambayo nilikua naifahamu Baba Levo siku zote amekua mtu wa utani mwingi, na kwa uelewa wangu pia amekua akitumia utani huo pia kufikisha ujumbe wake kwa alomdhamiria, na kwa aliyetumiwa ujumbe pia ataupata pengine huku akiwa anacheka. Nani atasahau matani yake kwa Peter Msechu juu ya uzito wake uliopitiliza ambao pengine unahatarisha maisha yake. Baba Levo amekua mstari wa mbele kumbukusha Peter hilo. Pia kuna ishu za yeye kuwa ‘Chawa’ wa baadhi ya wasanii na viongozi. Lakini pia yeye ni KIONGOZI ambaye wananchi wamemchagua, na chama cha ACT kiliridhia yeye kuwakilisha Chama, hilo si jambo ya mzaha na bila ya shaka anahitaji heshima kuliko ile ambayo tunamuonyesha ingawa pengine jinsi yeye binafsi navyojijeba ndo kunatufanya tumchukulie hivyo, lakini haiondoi heshima na uaminifu ambao Chama chake kilimpa pamoja na uaminifu kwa kuwatumikia wananchi wa Kigoma kule, kama diwani wao walompa dhamana. Baba Levo pia ashawahi kuingia matatani kwa ugomvi wake na dola baada ya kuvunja sheria za barabarani, kisa ambacho kilimfanya akae jela kwa takriban miezi mitano. Mengi sana yalikua yanahitaji uchambuzi na ufafanuzi, na kujuana pia kati yangu na yeye. Maongezi yetu yalikua kati ya muuliza maswali na mtoa majibu ambae alikua ana maelezo yake mengi sana na kwa hilo namkubali sana. Tumeongea kuhusu Siasa, muziki, familia, uongozi na marafiki. Yangu matumaini una enjoy kama ambavyo nami nili enjoy na kujifunza kutokana na maongezi haya. Nakutakia kheri na tafadhali enjoy. Love, Salama. Soundtrack Yeah by @MarcoChali /watch/QLnf4BH1euC1f Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

Category

Show more

Comments - 695