Duration 32:10

Salama Na Lord Eyes Ep 20 | HAWATUWEZI Part 1

91 856 watched
0
1.2 K
Published 15 Jun 2020

#YAHStoneTown #SalamaNa #PodCast SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm� �� ‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru� �� GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack ‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa Isaac ndo jinsi jina lake linavyoandikwa, kipaji adhimu kabisa kutoka Kaskazini mwa Tanzania, Allah kamjaalia kila ambalo msanii anaomba abarikiwe nalo wakati anapewa kipaji. Mrefu, muonekano mzuri, mashairi ya kibabe na kujiamini kulikokaa sehemu yake haswa. Walipoanza kama kundi hapo ndo attention yangu waliipata wana Nako 2 Nako Soldiers kutoka Ara, kila kitu kilikua tofauti juu yao, mavazi, style, matamshi na hata muonekano. Hii ilikua chachu ya kuwafikisha popote ambapo walikua wamepalenga. Mashabiki kila kona ya Tanzania na Afrika na dunia kwa ujumla, hakuna radio utakayoskilizia ambayo walikua hawapati nafasi. Walikua marafiki wa kila kituo na kazi yao waliifanya vizuri haswa. Nia ya mazungumzo haya ilikua ni ku catch up na rafiki yangu Isaac aka Lord Eyes aka Lodii. Kiasi cha heshima nilichokua nacho juu yake ni cha hali ya juu, uwezo wake wa kufanya kazi aliyopewa kipaji na Jalali ni wa kipekee. So nini kilienda kombo haswa kwa baadhi ya wanachama katika kundi lake na kwake yeye binafsi? Niamini haikua kazi rahisi kuweza kupata ujasiri wa kutaka kuyajua yote. Ni ngumu wakati mwingi kumuuliza mtu kuhusu struggle zake ambazo bado anapigana nazo na hii haijalishi hata kama mmezoeana kiasi gani. Lodii alikua hana cha kujificha, hana kinyongo wala hana kisasi na mtu yoyote, kubwa analolifanya ni kuwa bora one day at a time na kuelekea kwenye sehemu salama anayotaka kufika. So nini haswa kilitokea kwa Wanako? Na yeye alijikutaje kazama kwenye dimwi na madawa na maisha ambayo alikua hayataki? Siku ya kwanza kuonja ilikua lini? Na je ni lini alikua ana tatizo na akaanza kulifanyia kazi? Wazazi wake? Ana mtoto au watoto? Ni mapenzi yakimfikisha huko? Au marafiki? Au maisha? Na pia aliwezaje kutoka huko? Lini aliona haswa kama imetosha na basi aanze kujikomboa? Kusema za ukweli story ni ndefu ila tulipata wa kutusimulia na yangu matumaini kuna mambo mawili matatu utajifunza juu ya maisha, umaarufu, marafiki na maamuzi ambayo unaweza ukafanya. Tafadhali enjoy. Love, Salama Soundtrack Yeah by @MarcoChali /watch/QLnf4BH1euC1f Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

Category

Show more

Comments - 208