Duration 1:12

Karunguyeye Mnyama Mdogo

11 349 watched
0
38
Published 31 Aug 2021

Ndio, ni Karunguyeye. Kwa jina la kisayansi akijulikana kama Atelerix albiventris. Ni kiumbe mdogo yupo katika kundi la mamalia, mwenye ngozii yenu miiba eneo kubwa la juu ya mwili wake. Ni mnyama asiyeonekana mara kwa mara lakini ni maarufu sana miongoni mwa wengi wetu. Pia ni mmoja wapo ya wanyama wajishughulishao zaidi hasa nyakati za usiku na kupumzika nyakati za mchana. Pamoja na macho yake kuona vizuri hasa nyakati za usiku Karunguyeye hutumia pua yake ndefu yenye hisia katika kufanikisha mawindo yake. Vitoweo wake ni wadudu kama vile jongoo, Tandu, Buibui, Njenje na kadhalika; pia hupenda kunywa maji. Karunguyeye ni rafiki wa binadamu. Wakati mwingine usikiapo sauti hii usisite kusema ni Karunguyeye! Jina langu naitwa Jefta Riwa Na leo tulikuwa tukimuangalia Karunguyeye Hadi wakati mwingine na kwaheri. Mtayarishaji: Jefta Riwa Music: Royalty Free Music from Bensound https://www.bensound.com/royalty-free-music/track/straight

Category

Show more

Comments - 13