Duration 14:16

MGONJWA wa SELI MUNDU APONA kwa MAOMBEZI YA Mwl JULIUS K.NYERERE - ArkiASKOFU YUDA THADEUS RUWAICHI

431 watched
0
6
Published 16 Oct 2021

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam alishuhudia kumuona Binti Mgonjwa wa Seli Mundu aliyeshiriki pamoja na Wazazi wake Kumuombea kupitia Maombezi ya Mtumishi wa Mungu Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere kwamba Amepona. Aliwaomba wazazi hao kupata taarifa sahihi kutoka kwa Madaktari wake ili taarifa hizo zipelekwe kwa wanaohusika na Uchunguzi wa Tunu na Fadhila za Mwl Nyerere ili kutambuliwa kama MwenyeHeri. Aliyasema hayo siku wa Kumbukizi ya Mwl Nyerere 14.10.2021 huko Kibaha kwa Masista wa Shirika la Jimbo la Dada Wadogo wa MT FRANCISCO WA ASSIZI. Alitumia fursa hiyo kuwaalika Watanzania kumuomba Mwl Nyerere awaombee kwa Mungu wakiwa na Shida zao Mbalimbali na mwenye kupata zawadi ya majibu asisite kwa kufuata utaratibu kuwajulisha walio katika Uchunguzi huo ili ikifaa Baba wa Taifa aje kutambulika kama MWENYEHERI.

Category

Show more

Comments - 1