Duration 4:28

Sikiliza VIMBWANGA Vifupi vya Kamanda Lissu Tanganyika na Zanziba

539 364 watched
0
1.2 K
Published 15 Apr 2014

Sikiliza VIMBWANGA Vifupi vya Kamanda Lissu Tanganyika na Zanzibar ilivyochakachuliwa...!!! Dodoma/Dar. Mjumbe wa Bunge la Katiba, Tundu Lissu amesema Tanganyika ilikufa kwa amri iliyotolewa na Mwalimu Julius Nyerere na siyo kwa makubaliano katika hati ya Muungano. Huku akinukuu maneno yaliyopo katika vitabu vilivyoandikwa na Profesa Issa Shivji na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa, Lissu alisema Jamhuri ya Muungano ilizaliwa bila uhalali wa kisheria kwa kuwa hayakuwapo makubaliano ya kila upande wa Muungano. Alisema Aprili 26, 1964 (Siku ya Muungano), Mwalimu Nyerere alitoa amri ya masharti ya mpito ya mwaka 1964 ambayo pamoja na mambo mengine iliifuta Tanganyika. Akichambua kitabu cha '50 Years of Independence: A Concise Political History of Tanzania' (Miaka 50 ya Uhuru: Historia fupi ya Tanzania), kilichoandikwa na Msekwa na kuchapishwa Januari mwaka huu, Lissu alisema: "Msekwa anasema katika kitabu hicho kuwa amri hiyo ilichapishwa katika Gazeti la Serikali la siku hiyo. Kwanza, iliwabadilisha waliokuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika kuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano." Soma Zaidi: http://swahilivilla.blogspot.com/2014/04/tundu-lissu-atikisa-bunge.html

Category

Show more

Comments - 132